Halmashauri Mufindi yapitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi

Halmashauri Mufindi yapitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi

Halmashauri ya Mufindi Mkoni Iringa imepitisha Mpango wa Matumizi ya Ardhi kwa vijiji vinne vinavyofanyiwa Mpango huo na Shirika la PELUM Tanzania kwa kushirikiana na shirika wanachama la TAGRODE kupitia mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika sekta ya kilimo (CEGO) kwa ufadhili wa watu wa Marekani (USAID).

Akibainisha vijiji hivyo Jeswald Ubisimbali Mkuu wa Idara ya Ardhi na Makazi wilaya ya Mufindi alisema kupita kwa mipango hiyo ya ardhi kwenye vijiji vya Magunguli, Isaula, Usokami na Ugesa si tu itasaidia kumaliza migogoro ya Ardhi katika maeneo husika lakini pia imesaidia kuongeza idadi ya vijiji vilivyo fanyiwa mpango wa matumizi ya Ardhi.

“Kumekuwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Mufindi baina ya wakulima na wafugaji, wakulima kwa wakulima na zaidi migogoro baina ya wananchi na wawekezaji wakubwa jambo linalochangia kuzorotesha maendeleo hivyo kupita kwa Mipango ya matumizi ya Ardhi kwenye vijiji hivi vitano ni sehemu ya mafanikio makubwa kwa Wilaya na hii itasaidia kumaliza kero za migogoro kwenye maeneo husika kwani kwa kila kijiji vipande zaidi ya 500 vimepimwa vinavyojumlisha makazi, mashamba na Taasisi”.

Upitishwaji wa mipango hiyo ya matumizi ya Ardhi inaenda samabamba na ugawaji wa hatimiliki za kimila. “Kwa sasa baada ya mipango hii kupita, tunatarajia zoezi la uaandaaji wa hati za kimila kwa wanananchi wote waliopimiwa makazi na mashamba yao ikiwemo Tasasisi litakamilishwa na wenzetu wa PELUM Tanzania na hati hizo kupewa wahusika kama sehemu ya kuonyesha umiliki halali wa maeneo yao wenyewe.” Alifafanua Ubisimbali.

Jingine ni kuongezeka kwa idadi ya vijiji vilivyofanyiwa Mpango wa matumizi ya ardhi. Ubisimbali amebainisha kuwa mbali na Wilaya ya Mufindi kuwa na vijiji 121 lakini ni vijiji 43 tu ndio vimefanyiwa Mpango wa matumizi ya Ardhi na hivyo kuomba Shirika la PELUM Tanzania kuendelea kutafuta miradi mingine ili kuweza kusaidia vijiji vingine vilivyobaki.

Alisema kutokufanyika kwa matumizi ya Ardhi kwenye vijiji vilivyobaki inasababishwa na Halmashauri kuwa na bajeti finyu ikiwemo ukusanyaji wa mapato kutokufikia malengo jambo linalochangia kuendelea kuwepo kwa migogoro ya ardhi kwenye baadhi ya vijiji wilayani humo.

Ubisimbali alifafanua kuwa kwa sasa kuna vijiji 13 vilivyopo kwenye migogoro mikubwa ya ardhi baina  ya wananchi na wawekezaji ambao ni Kampuni ya Pareto, Mufindi Paper Mills, Green Resource Limited na SAO HILL FOREST na kusema kwa sasa migogoro hiyo inashughulikiwa ili kuweza kumaliza sitofahamu iliyopo  baina ya wananchi na wawekezaji hao kwani uendelevu wa migogoro hiyo inachangia kuzorota kwa maendeleo wilayani humo.

Mbali na kusisitiza njia sahihi ya kumaliza migogoro ya ardhi eneo lolote ni kufanyika kwa Mipango ya matumizi ya Ardhi kwani hilo litawezesha kufahamu ardhi ya kijiji iliyopo kama inakidhi mahitaji ya wananchi husika ama la na nini kifanyike.

Lakini pia aliwaasa wananchi toka vijiji hivyo vitano vya mradi kuwa wanapaswa kufuata na kutumia mpango jinsi walivyouandaa na kuupitisha pasipokupindisha sheria walizojiwekea na adhabu kali zifuatwe pindi mwananchi atakapokosea kulingana na sheria ndogondogo walizojiwekea.

Wilaya ya Mufindi ni moja kati ya Wilaya sita nufaika za mradi toka Mikoa mitatu (Morogoro, Dodoma na Iringa)yenye jumla ya vijiji 30 vilivyopo kwenye mradi unaotekelezwa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mashirika wanachama ambayo ni TAGRODE-Iringa, UMADEP-Morogoro na INADES-Dodoma.

 

Our Vision

Prosperous smallholder farmers deriving livelihoods from ecological agriculture

Our Mission

To strengthen capacity of Member Organizations in ecological agriculture for improved smallholder farmers’ livelihood

Our Core Values

  • Accountability
  • Transparency
  • Integrity